Deuteronomy 12:7-12

7 aHapo, katika uwepo wa Bwana Mwenyezi Mungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababu Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewabariki.

8 bMsifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe, 9 ckwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambao Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa. 10 dLakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi Bwana Mwenyezi Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama. 11 eKisha kuhusu mahali Bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtolea Bwana. 12 fHapo furahini mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wenu, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, pamoja na Walawi kutoka miji yenu ambao hawana mgawo wala urithi wao wenyewe.
Copyright information for SwhKC